×

Dakika 125 za Saido Yanga, Zavunja Rekodi

BALAA aliloanza nalo kiungo mshambuliaji mpya wa Yanga, Said Ntibazonkiza ‘Saido’ sio la kitoto unaambiwa, kwani nyota huyo amevunja rekodi za mastaa wote wa kimataifa waliosajiliwa na Yanga msimu huu.

 

Akitumia dakika 125 tu ndani ya jezi ya Yanga kwenye michezo miwili aliyoichezea nyota huyo amefanikiwa kuhusika kwenye mabao manne ya Yanga akifunga mabao matatu na kuasisti bao moja, jambo ambalo hakuna staa yeyote wa Yanga amefanikiwa kulifanya msimu huu ndani ya michezo miwili mfululizo.

 

Anakuwa ni mchezaji pekee wa Yanga kufanya mambo makubwa akitumia dakika chache zaidi Saido aliyekamilisha usajili wake na kutambulishwa na Yanga, Oktoba 11, mwaka huu, alitumia dakika 80 kuichezea Yanga kwa mara ya kwanza kwenye mchezo wa kirafi ki dhidi ya Singida United uliopigwa kwenye Uwanja wa Liti mkoani Singida na kufanikiwa kufunga mabao mawili.

 

 

Juzi Jumamosi alifunga bao moja na kuasisti bao moja kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Dodoma Jiji mkoani Arusha akicheza kwa dakika 45 tu.

 

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Saido alisema: “Nashukuru kwa upendo mkubwa ambao Wanayanga wamenionyesha tangu nimejiunga na klabu hii, sapoti yao inanifanya niwe na deni kubwa la kufanya kazi inayoeleweka uwanjani.

 

“Nami niwahakikishie kuwa nitafanya kila kilicho ndani ya uwezo wangu kuhakikisha Yanga inafi kia malengo ya kutwaa ubingwa msimu huu.”

JOEL THOMAS, Dar es Salaam

 

Leave a Comment