
Klabu ya Barcelona na Arsenal wametinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya huku Arsenal wakitinga kwa mara ya kwanza baada ya miaka 14 kufuatia ushindi wa penalti 4-2 dhidi ya FC Porto.
Dakika 90 zilimalizika Arsenal wakiwa mbele 1-0 ikiwa ni sare ya jumla ya 1-1 kufuatia kipigo cha 1-0 kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza.
Muda wa ziada haukuzaa goli hali iliyopelekea mchezo kuamuliwa kwa mikwaju ya penalti.
Pia Barcelona imetinga hatua hiyo kufuatia ushindi wa jumla wa 4-2 dhidi ya Napoli kwenye hatua ya 16 bora.
Barcelona imetinga robo fainali kwa mara ya kwanza tangu msimu wa 2019/20.