×

Wachezaji Simba Waapa Zimbabwe

WACHEZAJI wa Simba wameapa kuondoka na ushindi katika mchezo wao wa kwanza wa raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya FC Platinum, unaotarajiwa kuchezwa keshokutwa Jumatano nchini Zimbabwe.

 

Simba wamefuzu raundi ya kwanza, mara baada ya kufanikiwa kuiondoa timu ya Plateau United kutoka Nigeria katika raundi ya awali ambapo kama watafanikiwa kuwaondoa FC Platinum watatinga hatua ya makundi.

Akizungumza na Championi Jumatatu, beki wa kati wa timu hiyo, Pascal Wawa, alisema kuwa wanatarajia kufanya vyema katika mchezo huo kwani malengo yao ni kuhakikisha wanasonga mbele zaidi ya walipofika kwa sasa kwenye michuano hiyo.“

Tunatarajia kuona kuwa tunafika mbali zaidi ya hapa na haya ni malengo ya Wanasimba wote, hivyo tutahakikisha tunafanya vyema ili kuyafikia malengo yetu haya, ushindi tukiwa ugenini litakuwa jambo muhimu zaidi kwa upande wetu.”

Naye Ibrahim Ame alisema kuwa: “Tunatarajia kupata upinzani mkubwa zaidi kutoka kwa wapinzani wetu, hivyo kama timu tunahitaji kupambana ili kupata matokeo chanya kwa upande wetu ambapo ushindi ndio jambo zuri kulingana na malengo yetu.”

STORI: MARCO MZUMBE,Dar es Salaam

Leave a Comment