×

Breaking: Waliomuua Alphonce Mawazo Wahukumiwa Kifo

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Mwanza leo Desemba 24, 2020, imewahukumu washtakiwa wanne katika kesi ya mauaji ya aliyekuwa mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo, adhabu ya kifo baada ya mahakama kuwatia hatiani kwa  kosa la mauaji ya kukusudia.

 

Washtakiwa hao ni Alfan Apolnari, Epafra Zakaria, Hashim Sharifu na Kalulinda Bwire ambao walikuwa wakikabiliwa na mashtaka ya kutekeleza mauaji hayo Novemba 14, 2015, katika mji mdogo wa Katoro wilayani Geita, siku moja kabla ya uchaguzi wa udiwani katika kata ya Ludete.

 

Mawazo aliuawa siku chache baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ambapo aligombea ubunge Jimbo la Busanda.

Leave a Comment