×

Tayari New Zealand, Australia Washerehekea Mwaka Mpya

WAKATI barani Afrika ikiwa bado ni mchana (wakati wa kuandika habari hii), nchini New Zealand na Australia ambako ni mashariki mwa bara hili, wakazi wake tayari wamesherehekea kuanza kwa mwaka mpya wa 2021 wakiachana na mwaka 2020 ulioleta janga la ugonjwa ulioenea dunia nzima — Covid-19.

 

 

Nchi hizo na visiwa vilivyoko katika Bahari ya Pacific ikiwa ni pamoja na sehemu ya Russia, tayari zimesherehekea kuingia kwa mwaka mpya.

 

 

Nchini New Zealand, ambako ni watu 25 tu wamekufa kutokana na ugonjwa wa Covid-19 na ambako hakuna masharti dhidi ya wananchi katika kuzuia kusambaa kwake, makundi ya watu yameonekana katika mitaa mbalimbali yakisherehekea na kulipua baruti angani.

Nchini Australia ambako ugonjwa huo umedhibitiwa, wananchi wameonekana wakisherehekea katika miji ya Melbourne na Sydney.

 

 

Kwa walimwengu wapatao bilioni saba, kuna sehemu ambako sherehe hizo zitafanyika majumbani tu au kutofanyika kabisa hususan mitaani.

 

 

Huko Ufaransa, Latvia na Brazil, polisi na wanajeshi wamejitayarisha  kuhakikisha  watu wanafuata masharti ya kutotoka nje na kutofanya mikusanyiko.  Hii ni kutokana na kwamba nchi nyingi bado wananchi wake wamezuiwa kutoka nje ya makazi yao na kwamba chanjo za ugonjwa huo ndiyo kwanza zimeanza kutolewa.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Leave a Comment