
MBUNGE wa Jimbo la Buchosa, Mhe. Eric Shigongo, ametembelea barabara ya Kasheka iliyokatika kutokana na uzembe wa Mtendaji wa Kijiji hicho kutokana na kushindwa kusimamia ujenzi wa karavati zilizosombwa na maji na kusababisha kukatika kwa mawasiliano ya barabara hiyo.
Kutokana na hali hiyo Shigongo aliamua kumpigia simu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Buchosa na kuomba amuhamishe kituo cha kazi mtendaji huo kwani hawezi kufanya kazi katika jimbo hilo.