×

Kiba Aanika Ukweli Kuachamuziki

BAADA ya maneno mengi kusambaa mitandaoni kuwa Mfalme wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ yupo mbioni kuacha muziki, hatimaye mwenyewe amefungukia ukweli juu ya ishu hiyo, Gazeti la IJUMAA WIKIENDA linakupakulia.

 

Mshtuko kuhusu mfalme huyo wa muziki wa Bongo Fleva kuacha muziki uliibuka wiki chache zilizopita na kusababisha mioyo ya baadhi ya wapenzi wa burudani ndani na nje ya Bongo isinyae kutokana na utamu wa ngoma za msanii huyo aliyeipeperusha vyema bendera ya Tanzania kimataifa kupitia tasnia hiyo ya muziki.

 

Hata hivyo, katika mahojiano maalum (exclusive interview) ambayo King Kiba amefanya na Gazeti IJUMAA WIKIENDA, ameweka wazi kuwa, si kweli kwamba anatarajia kuacha muziki.

Kiba amekwenda mbali zaidi na kueleza kuwa madai hayo yalikuwa stori za mitandaoni hivyo mashabiki wake watambue kuwa si habari za kweli.

 

Uvumi wa Kiba kuacha muziki umeshika kasi ikiwa ni miezi michache imepita tangu msanii mwingine nguli katika uwanja wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee ‘Vee-Money’ naye kutangaza kuacha muziki, jambo ambalo liliibua mjadala mkubwa ndani ya jamii.

Aidha, mbali na masula hayo ya kuacha muziki, Kiba amezungumzia pia suala la kuachana na mkewe, Amina Khaleef kwa mara nyingine tena ambapo alifunguka kama ifuatavyo;

 

IJUMAA WIKIENDA: Mambo Kiba…

KIBA: Poapoa, niambie…

IJUMAA WIKIENDA: Ulijisikiaje kutajwa kwenye orodha ya billboard kama mmoja wa wasanii 10 waliofanya vizuri kwa mwaka 2020?

KIBA: Nilijisikia vizuri sana.

 

IJUMAA WIKIENDA: Umevunja rekodi kwa kufikisha watazamaji (viewers) milioni 1 ndani ya saa 24 kupitia wimbo wako na DJ SBU, unajisikiaje?

 

KIBA: Ninajisikia vizuri pia, lakini vilevile nimefanya muziki tofauti na kazi zangu nilizowahi kufanya; yaani hii ngoma (Nakupenda aliyofanya na DJ SBU wa Afrika Kusini) ina ‘vaibu’ la klabu la kutosha, tofauti na kwenye ngoma nyingine ambazo huwa tunafanya vitu kama hivi mara mojamoja sana. Kwa hiyo hii inaonesha mabadiliko makubwa kwenye muziki wangu pia.

 

IJUMAA WIKIENDA: Ilikuwa na urahisi au ugumu kiasi gani kufanya kazi na DJ SBU wa Afrika Kusini?

KIBA: Hakukuwa na ugumu wowote, kulikuwa na urahisi sana kwa sababu tulikutana mara ya kwanza kwenye biashara ndipo tukaona kuna fursa pia ya kufanya muziki.

IJUMAA WIKIENDA: Tangu uachie album yako ya Cinderella mwaka 2009 ni miaka mingi imepita, vipi una mpango wowote wa kuachia album nyingine 2021?

 

KIBA: Ndiyo; album yangu ya mwisho niliitoa mwaka 2009 na sasa hivi nina mpango wa kuachia album nyingine kipindi cha hivi karibuni na haitafika hata mwezi wa sita (2021).

IJUMAA WIKIENDA: Mbali na kuachia album una malengo gani mengine kwenye muziki wako kwa mwaka 2021?

 

KIBA: Kwa kweli siwezi kuelezea malengo yangu mwaka huu yapoje, lakini nitahakikisha kwamba nitasimama zaidi na zaidi na kuzidi kupanda tu siyo kushuka, lakini pia kuinua vipaji vipya kwenye gemu.

Ila kuna malengo mengine siwezi kusema kwa sababu ni kama unawapa ‘aidia’ watu wengine.

 

IJUMAA WIKIENDA: Mwaka 2020 ulikuwa wa aina gani kwako?

KIBA: Asilimia 60 ulikuwa vizuri, lakini asilimia 40 uliathiriwa na Corona.

IJUMAA WIKIENDA: Ni jambo gani baya ambalo hutalisahau kwa mwaka 2020?

 

KIBA: Sitasahau huu ugonjwa wa COVID 19 ambao unasabishwa na kirusi cha Corona kwa sababu ulifanya mambo mengi yasimame.

IJUMAA WIKIENDA: Kuna tetesi kwamba mwaka huu una mpango wa kuacha kufanya muziki hili limekaaje?

KIBA: Duh! Hizo ni stori tu hakuna kitu kama hicho…

 

IJUMAA WIKIENDA: Ni kweli kwamba haupo kwenye uhusiano mzuri na mkeo, Amina?

KIBA: Kwa nini unahitaji kujua kuhusu maisha yangu?

IJUMAA WIKIENDA: Kwa sababu wewe ni staa na unafuatiliwa na watu wengi na hata ndoa yako pia ipo mitandaoni, lakini mbali na hilo hizi ni tetesi ambazo zinasambaa sana mitandaoni, hivyo mashabiki wako wanatamani kusikia lolote kutoka kwako, je, ni kweli au la?

STORI: MEMORISE RICHARD, DAR

Leave a Comment