




Timu ya Masoko kutoka Kampuni ya Global Group kupitia magazeti ya Championi na spotiXtra imeingia mtaani na maeneo ya Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam kwenye michuano ya ligi ya mabingwa Afrika, Simba SC na FC Platinum ya Zimbabwe ambapo mchezo huo niwa pili wa Raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Hii imekuwa kawaida ya Kampuni ya Global Publishers kurudisha fadhila kwa wasomaji wake ikiwa ni pamoja na kuwapa zawadi mbalimbali.
“Hii imekuwa desturi kurudisha fadhila kwa wasomaji wetu kwani wamekuwa wakituunga mkono sana, hivyo ni jambo jema kuwarudishie kile tunachokipata kutoka kwao, ili na wao wajisikie kama familia ya Championi na Spoti Xtra,” alisema Anthony Adam ambaye ni Mkuu wa Idara ya Usambazaji wa Global Publishers wakati wakigawa tiketi hizo kwa mashabiki.