×

Polisi Watano Wakamatwa kwa Tuhuma za Uhalifu JNIA

 

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene ameagiza maofisa watano wa polisi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kuchukuliwa hatua za kinidhamu baada ya intelijensia yake kubaini wanajihusisha na matukio ya ukiukwaji wa maadili.

 

Simbachawene alitoa kauli hiyo jana Januari 9, wakati wa ziara yake katika vikosi mbalimbali vya Jeshi la Polisi Kanda ya Dar es Salaam kwa lengo la kukagua na kutathmini utendaji kazi, alisema Serikali itaendelea kuwachukulia hatua za kinidhamu wanaochafua heshima ya jeshi hilo.

 

Waziri Simbachawene alisema amebaini maofisa hao wanajihusisha na mtandao wa kusafirisha mabinti kwenda kufanya kazi za ndani katika nchi za uarabuni na kutumia nafasi zao kutapeli baadhi ya abiria.

 

“Nimewataja kwa majina na nimewakabidhi hawa viongozi na tutawachukulia hatua za kinidhamu kwa sababu tuna taarifa za kiintelijensia wanafanya vitendo hivyo ikiwamo kubabaisha abiria wakati wa kuondoka, wakiona abiria huyu ana uwezo wa kifedha wanafanya ubabaishaji,” alisema.

 

Hata hivyo, Kamanda wa Kikosi cha Viwanja vya Ndege nchini, Jeremia Shila aliyepokea agizo hilo alisema kuwa hatua itakayofuata kwa sasa ni uchunguzi ili kujiridhisha,  “kwa sasa maofisa hiyo wataendelea kuwa kazini hadi ushahidi wa tuhuma hizo utakapokamilika”.

Leave a Comment