×

Magufuli Aitaka Wizara Kuanza Uchimbaji Nickel Haraka – Video

RAIS John Magufuli leo Jumanne Januari 19, 2021, ameitaka Wizara ya Madini kuhakikisha makubaliano kati yake na kampuni ya LZ Nicol yanatekelezwa kwa muda mfupi ili mradi wa uchimbaji wa madini wa Kabanga uanze kutekelezwa.

 

Akizungumza  katika hafla ya utiaji saini makubaliano hayo, amesema kuchelewa kwa mradi huo kunaifanya wilaya ya Ngara kuendelea kuwa masikini wakati kuna rasilimali.

 

“Watanzania wamesubiri kwa muda mrefu wamechoka wanataka mradi huu uanze. Michakato Watanzania wameshachoka nayo, mmetuleta hapa na mimi nilikuwa nawaangalia tu, tunataka mtambo wa uchenjuaji uanze kujengwa.

 

“Mgodi huu ukianza mapema nitakuwa na uhakika wa ongezeko la ajira hususani wananchi wa Ngara ambao wamekaa na umaskini kwa muda mrefu wakati wamekalia mabilioni. Madini haya ni mali ya wananchi wa Kabanga, wanakaa kwenye mali wakati wao ni maskini,” amesema.

 

Amewasisitizia wawekezaji kuwa Tanzania ni salama hivyo wasisite kuja kuwekeza nchini.

 

“Tanzania ni nzuri ina upendo na wananchi wake ni wachapakazi. Nimefurahi kuhusu kauli ya makamu mwenyekiti wa LZ Nicol kuwa faida itakuwa nusu kwa nusu. Lazima tufaidi wote, nitoe wito kwa wawekezaji kuwa Tanzania ni sehemu sahihi ya uwekezaji, waje kila madini yapo,” amesema.

Leave a Comment