
METACHA Mnata, kipa namba moja ndani ya Yanga, amesema kilicho nyuma ya mafanikio yake ndani ya kikosi hicho ikiwa ni pamoja na kutofungwa kwenye dakika 990 ni ushirikiano wa wachezaji wenzake pamoja na maombi.
Mechi 17 ambazo ni sawa na dakika 1530, kipa huyo amekaa langoni msimu huu katika Ligi Kuu Bara na mechi 11 hakuruhusu bao, akiwa ni kinara wa clean sheet ndani ya ligi hiyo msimu huu.Anafuatiwa na Daniel Mgore wa Biashara United mwenye clean sheet 10 kati ya mechi 15 alizokaa langoni.
Metacha ni chaguo la kwanza chini ya Kocha Mkuu, Cedric Kaze raia wa Burundi, amekuwa akimuweka benchi kipa Faroukh Shikhalo ambaye amecheza mchezo mmoja na kuruhusu bao moja.
Kipa huyo amesema: “Kikubwa ambacho kinanifanya ninakuwa bora ni ushirikiano ambao ninaupata kutoka kwa wachezaji wenzangu pia huwa ninaomba kwani nina amini katika Mungu.