×

Mashine Mpya Yatambulishwa Simba

KLABU ya Simba imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa zamani wa Esperance YA Tunisia, ambaye ni raia wa Nigeria Junior Lokosa ambapo leo Januari 25, kupitia ukurasa wao kwenye mtandao wa  Instagram umemtambulisha rasmi mshambuliaji huyo.

 

Kwa mujibu wa timu ya  Simba lengo kuu ni nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika huku lengo Mama likiwa Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho hivyo wanaamini atawasaidia kufikia malengo hayo.


Lokosa ana kazi kubwa kupigania namba kwani tayari wapo washambuliaji wengine Meddie Kagere, John Bocco, Chris Mugalu.

Nyota huyo ataanza anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi kitakachoshiriki Simba Super Cup itakayoanza kutimua vumbi Jumatano Januari 27.

Leave a Comment