
KIPA wa Klabu ya Real Valladolid inayoshiriki Ligi Kuu ya Hispania (La Liga), Andriy Lunin, ameomba kumuoa mpenzi wake, Anastasia Tamazova kwa staili ya aina yake.
Kipa huyo ambaye anacheza kwa mkopo klabuni hapo akitokea Real Madrid, aliamua kupiga goti uwanjani baada ya sare ya 1-1 dhidi ya Valencia hivi karibuni na kuomba ndoa kwa Anastasia.
Kipa huyo baada ya mechi, alimuita mpenzi wake uwanjani, akampigia goti akiomba ndoa katikati ya Uwanja wa Jose Zorrilla.
“Nilisema ndiyo. Nakupenda sana Andriy Lunin,” aliandika Anastasia kwenye Instagram, akiambatanisha na picha ya kipa huyo akiwa amempigia goti akiomba ndoa.
BARCELONA, Hispania