
MKURUGENZI wa Uwekezaji wa Kampuni ya GSM ambao ni wadhamini wa Yanga, Injinia Hersi Said, amefunguka kuwa shabaha yao katika usajili mkubwa walioufanya msimu ni kuhakikisha kikosi hicho kinashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.
Yanga juzi ilifunga dirisha la usajili kwa kumshusha mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Fiston Abdoul Razak aliyesajiliwa kama mchezaji huru baada ya kuachana na ENPPI ya nchini Misri aliyokuwa akitumika tangu msimu uliopita.
Licha ya kusajili wa kama mchezaji huru, Fiston amekuwa akiitwa ndani ya kikosi cha timu ya taifa ya Burundi ambapo kwenye michezo ya kufuzu AFCON amefanikiwa kuifungia Burundi mabao sita na kukamatia nafasi ya pili kwenye chati ya wafungaji bora akifungamana na nyota wa timu ya Taifa ya Nigeria, Odion Ighalo anayekipiga Manchester United.
Akizungumza na Spoti Xtra, Injinia Hersi alisema: “Tumekamilisha usajili wa Fiston, miongoni mwa washambuliaji bora zaidi katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati.“
Shabaha yetu katika kufanya usajili huu ni kuhakikisha tunakuwa na kikosi ambacho kitatwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu, na kupata nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.“Tunaamini Dickson Job pamoja na Fiston