×

Mwigizaji Mkongwe Hashim Kambi Afariki Dunia Dar es Salaam

Mwigizaji mkongwe wa filamu nchini Tanzania, Hashim Kambi, amefariki dunia leo, tarehe 27 Aprili 2026, nyumbani kwake eneo la Sinza, jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa za awali kutoka kwa watu wa karibu, marehemu amefariki dunia asubuhi ya leo, huku chanzo cha kifo chake kikielezwa kuwa bado hakijathibitishwa rasmi na familia pamoja na wahusika wa afya. Taarifa zaidi zinatarajiwa kutolewa baada ya taratibu za awali kukamilika.

Hashim Kambi alijijengea jina kama mmoja wa waigizaji wa kizazi cha mwanzo waliosaidia kukua kwa tasnia ya filamu nchini Tanzania. Kwa miaka mingi, ameshiriki katika kazi mbalimbali za sanaa ya uigizaji, akionekana katika filamu na miradi ya maigizo ya televisheni iliyopendwa na watazamaji.

Marehemu alijulikana kwa uwezo wake wa kuigiza majukumu tofauti, hususan yale ya uhalisia wa maisha ya kawaida, jambo lililomfanya apendwe na mashabiki wengi wa filamu za Kitanzania.

Leave a Comment