×

Kifurushi cha Sumu Chakutwa Ikulu, Wasaidizi wa Rais Waugua Ghafla

 

WASAIDIZI wawili wa Rais wa Tunisia wameugua baada ya kufungua kifurushi kilichofikishwa katika ofisi yao kilichoshukiwa kuwa na sumu, taarifa ya ofisi ya rais imeeleza.

 

 

Taarifa inasema mkurugenzi wa ofisi ya rais alikifungua kifurushi hicho na hakukuta barua yoyote ndani yake. Hata hivyo, baada ya kukifungua  “afya yake ilianza kuwa mbaya, na alijihisi kama alikuwa anazimia, alikuwa pia na maumivu makali ya kichwa.”

 

 

Mfanyakazi mwingine alikuwepo wakati wa tukio, ambapo taarifa imeeleza pia kwamba alipata dalili kama hizo ‘’lakini hali haikuwa mbaya zaidi’’.

 

 

Bahasha ilichanwa kabla ya kufikishwa kwenye wizara ya mambo ya ndani, taarifa iliongeza. Haijulikani ndani ya bahasha hiyo kulikuwa na nini kilichosababisha athari kwa maafisa hao. Taarifa hiyo imesema vipimo vimechukuliwa na kupelekwa kwenye hospitali ya kijeshi ili kubaini sababu za maafisa kuonyesha dalili hizo.

 

Leave a Comment