×

JPM Azindua Maji ya Ziwa Victoria Kahama, Amsifu Waziri wa Maji – Video

RAIS  John Magufuli leo amezindua mradi wa maji wa Ziwa Victoria kwa ajili ya miji ya Kagongwa na Isaka mkoani Shinyanga, ambapo ameagiza kuanzia kesho wakandarasi waanze kutawanya maji vijiji vya maeneo ya karibu ili vianze kupata maji.

 

 

Amesema wizara iliyomtesa kwa miaka mitano ni Wizara ya Maji ambapo katika kipindi cha muda mrefu miradi iliyokuwa imekamilika haikuzidi 30%, huku akimwagiza waziri kuhakikisha miradi ambayo ilikuwa haijakamilika inakamilika kwani Watanzania wamechoka kusubiri wakati hawapati maji.

 

“Wanawake wameteseka kwa miaka mingi kwa shida ya maji, na wanaume wa hapa lazima waoge maji ya moto, saa nyingine kwa uhaba wa maji mwanamke anaenda kitandani wakati hajaoga huku mumewe akiwa ameoga kwa sababu alimuandalia kwanza.

 

“Watanzania wamechoka kusubiri miradi, nataka miradi ikamilike mapema na isiwe inazaa variation, nimeshukuru umeanza kuchukua hatua kwa wakandarasi feki waliokuwa Mwanga ukawafukuza kwa sababu ungechelewa kuwafukuza mimi ningekufukuza wewe.

 

“Nimeambiwa matenki haya yanajaa kwa lita milioni 1.6, maji yamejaa mle nina uhakika vijiji vinavyozunguka hapa havina maji, Mungu alitupa Ziwa Victoria serikali ya CCM imeweza kuyavuta, matenki haya hayana faida kama wananchi hawana maji.

 

“Huu mradi muutunze, haya maji yanapotoka Ziwa Victoria mpaka hapa ni gharama kubwa, msiyatumie kufyatulia matofali, haya maji yamechanganywa na dawa kwa ajili ya kuua wadudu, myatumie kwa ajili ya kupikia na kuoga, mwili unahitaji maji safi.

 

 

“Sitaki miradi kichefuchefu kwa sababu kichefuchefu mwisho wake ni kutapika na sitaki siku moja utapike, nataka miradi ya maji ikamilike.  Waziri nimefurahi umeanza kuchukua hatua kwa wakandarasi feki kule Mwanga ukawafukuza, ungechelewa ningekufukuza wewe.

 

 

“Na bamia mzilime kabisa, mama unapenda bamia kuzila, bamia ni tamu kweli kwa hiyo bamia, matango na kila kitu lima vitanunuliwa hapahapa kwenye barabara, mkijituma kulima baadaye mtaona faida yake kwa sababu mji huu wa Kahama unakua.

 

 

“Waziri wa Maji, wakandarasi wanaokuchelewesha fukuza tu, hawakuja huku kutangaza mambo ya mchezo, wamekuja kufanya kazi, ukitaka hela ya Tanzania lazima ufanye kazi, wakandarasi ambao umewafukuza kule Mwanga, wafutwe wasipate kazi yoyote Tanzania nzima,” amesema Magufuli.

 

Leave a Comment