×

Simba Wajifungia Kumjadili Fiston wa Yanga

BENCHI la ufundi la Simba limeonekana kupata hofu kubwa juu ya uwezo wa mshambuliaji mpya wa Yanga, Fiston Abdoul Razak na sasa wamemwekea kikao.

 

Bado mchezaji huyo hajaonekana kwenye mechi ya mashindano ya timu hiyo lakini kutokana na sifa zake na video zake ambazo zipo kwenye mitandao ya You Tube anaonekana kuwa mchezaji mahiri.

 

Juzi benchi la Simba lilikutana na kujadili mambo mengi ikiwemo michuano iliyomalizika ya Simba Super Cup, lakini moja ya jambo ambalo lilizuka ni ishu ya staa huyo raia wa Burundi.

 

Chanzo cha ndani kinasema kuwa kocha wa Simba alitaka kufahamu kuhusu wapinzani wake kwenye ligi na jinsi na Fiston lilikuwa moja ya jambo ambalo lilijadiliwa.

“Unajua kocha ana utaratibu wake mpya, mnaweza kukaa na akauliza kuhusu jambo ambalo hata hamkutegemea, sasa juzi kwenye kikosi wakati tunajadili mambo ya klabu kuna mmoja wa watu aliamua kuingiza suala la safu ya ushambuliaji wa timu pinzani kwenye ligi

 

“Lakini Fiston ndiye alionekana kujadiliwa zaidi kutokana na mmoja wa watu waliokuwa pale kumfahamu vyema na kuanza kumchambua, inaonekana ni mchezaji imara na mwenye uwezo, ingawa hawezi kututia shaka,” kilisema chanzo hicho.

 

Simba wanatarajiwa kucheza mchezo wao wa kiporo dhidi ya Dodoma Jiji kesho na Jumapili watarejea uwanja wa Taifa kuvaana na Azam FC.

Mwandishi Wetu

Leave a Comment