×

Erasto Nyoni: Sina Mpango wa Kustaafu

BEKI wa Simba, Erasto Nyoni amesema kuwa hana mpango wa kustaafu kucheza soka na kama atataka kuchukua maamuzi hayo basi atatoa taarifa mwenyewe.

 

Tetesi za Nyoni kustaafu ziliibuka baada ya kurudishwa kutoka Cameroon wakati alipokuwa na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars katika michuano ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (Chan), ikielezwa kuwa alikuwa na majeraha ambayo yalimfanya akose ushiriki katika michuano hiyo.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, mara baada ya kuulizwa kuhusu tetesi hizo, Nyoni alisema kuwa, watu waache maneno ya uwongo kwani hana malengo ya kustaafu kwa sasa.

 

“Mlishawahi nisikia nikisema nataka kustaafu? Basi nikihitaji kustaafu nitawaambia mimi mwenyewe sina haja ya kusemewa na watu,” alisema Nyoni.

Stori: Careen Oscar, Dar es Salaam

Leave a Comment