
WIKENDI iliyopita kulikuwa na sherehe tamasha la Tumewasha na Tigo, lililokuwa limeandaliwa na Wasafi Media. Tamasha hilo lililofanyika katika uwanja wa uhuru, watu kibao walijaa huku wasanii lukuki wakiperfome.
Mbali na hayo, kioja kilichoibua mjadala ni suala la msanii Raymond Mwakyusa maarufu kama Rayvan, kuzima stejini, kwamba alianguka vibaya wakati akicheza.
Kuanguka huko kulimsababishia maumivu makali kiasi cha kubebewa na Babalevo na wasaidizi wengine kisha kutolewa.
ZUCHU
Haya yanajiri wiki chache baada ya msanii mwenzake wa Wasafi, Zuhura Othman ‘Zuchu’ kuanguka jukwaani akitumbuiza.
Mwanamuziki huyo alikuwa anawatumbuiza mashabiki wake katika shoo mjini Dodoma, Tanzania wakati alijaribu kupanda kwenye mlingoti wa stegi kuonyesha uledi wake wa kudensi.
Mrembo huyo alipoteza mwelekeo na kuanguka chini kwa kishindo.Afisa wa jukwaa hilo alikimbia kumuokoa na kujaribu kumubeba, na katika kuonyesha alikuwa sawa, Zuchu alipanda tena na kufaulu kuonyesha densi yake.Baada ya kuchambwa na wafuasi, Zuchu kupitia mtandao wa kijamii, alichapisha picha yake akiwa ameshikilia pesa sikioni akipiga simu.
HARMONIZE
Agosti mwaka jana, msanii wa Bongo fleva, Rajabu Abdul ‘Hamonize’ alianguka vibaya wakati akiingia uwanja wa Taifa kwa mbwembwe za kijeshi.Harmonize ambaye aliingia kwa kutumia kamba mithili ya makondandoo alianguka na kuzua tafrani katika shoo hiyo ambayo ilikuwa ni wiki ya wananchi – Yanga.

DIAMOND
Disemba 9, mwaka 2018, Msanii wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul maarufu Diamond Platnumz, naye alianguka jukwaani wakati akitumbuiza katika Uwanja wa Nelson Mandela uliopo Sumbawanga mkoani Rukwa katika Tamasha la Wasafi (Wasafi Festival).
Kipande cha video kilichosambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii kilimuonesha Diamond akitumbuiza sambamba na msanii mwenzie kutoka Wasafi, Raymond Mwakyusa maarufu Rayvanny, wakiimba na kucheza wimbo wa Zilipendwa ndipo jukwaa lilishindwa kuhimili mikiki ya wasanii waliokuwa wakiruka ruka na kuvunjika na kisha kuangukia ndani ya jukwaa hilo la kutengenezwa.
Katika ukurasa wake wa Instagram, Diamond aliandika aliumia mkono katika tukio hilo na tayari amepaka dawa ya ‘spirit’.

H- BABA
Febaruari 24, Msanii wa Bongo Fleva, Hamis Ramadhani ‘H. Baba’ alipata ajali na kuanguka stejini wakati akiingia na swaga zake kwenye Tamasha la “JIPOZE NA TWIST” Mkoani Mbeya.
Baada ya kupata ajali hiyo aliandika ujumbe huu kupitia ukurasa wake wa Instagram: “Nimepata ajali jukwani nimetenguka kiuno hii style ni ngumu inaitwa slide nikipona sirudii tena kwa sasa nipo hospital #Asanteni sirudii tena nimekoma ? Slide slide slide sirudii, #Bado nipo hospital kiuno kimeteguka.”Wakati huo H baba alipost picha nyingine akitembea kwa kuchechemea akiwa anaugulia maumivu na kuandika kuwa “hali yangu bado ila Mungu
AKOTHEE
Mwaka 2019, Msanii Esther Akoth ‘Akothee’ kutoka Kenya naye wakati akitumbuiza jukwani mara ghafla alizimia na kudondoka.Kwa bahati nzuri walikuwepo watu karibu naye waliompa huduma ya kwanza na akaweza kurejelea fahamu zake.
LAVA LAVA
Mwaka 2018, katika Tamasha la Wasafi Festival mkoani Morogoro, Msanii Abdul Iddi ‘Lavalava’ naye akiwa stejini mara ghafla mrembo mmoja alipanda jukwani na akaanza kudensi nae huku anaimba.Yule dada akiona hamna tatizo kama akimpiga busu supastaa na mara boom, midomo ikakutana na wakabadilishana mate.Kilichofuatia ni Lava Lava kudondoka na kuzimia ghafla.
Alifanyiwa huduma ya kwanza na aliporejelewa na fahamu, kukazuka tetesi kwamba alikuwa akisaka kiki.Lakini Lava alijitetea kwa kusema hajui kilichosababisha hadi akazirai. Hajui kama ni lile busu lililomchizisha au ni kitu kingine.
PAPA WEMBA
Mwaka 2016, Mkongwe huyu wa muziki wa lingala ambaye sasa ni marehemu alikuwa akitumbuiza mjini Abijan, Ivory Coast alipodondoka ghafla na kuzirai.
Bendi yake ikawahi kumfanyia huduma ya kwanza lakini haikusaidia. Wakajaribu kumharakisha hospitalini lakini wakawa wamechelewa kwani Papa alikuwa tayari ameshafariki dunia.Papa alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 66. Tetesi zinadai kwamba alitiliwa sumu kwenye Mic yake aliyoipumua kipindi akiwa anatumbuiza na mara moja ikamdhuru na kumtoa uhai.
JUSTIN BEIBER
Mwaka 2013, Staa huyu alikuwa akipiga shoo katika uwanja wa London 02 Arena Uingereza. Mara ghafla alianza kulalamika kushindwa kupumua vizuri. Lakini licha ya kujihisi vibaya, alisisitiza kwamba lazima amalize kupiga shoo. Aliishia kula jeuri yake baada ya hewa kumkatikia ghafla na akazirai stejini. Alikimbizwa hospitalini ambapo alifanyiwa huduma ya kwanza na kuweza kurejeshwa kwenye ufahamu.
KELLY ROWLAND
Mwaka 2007 katika tamasha la ‘This Day Music Festival, Lagos’ Mwanamuziki huyu aliyepata umaarufu mkubwa na kundi la Destiny Child lililowajumisha vile vile Beyonce na Monica, naye aliwahi kuzirai stejini kipindi akiwa anatumbuiza.Kelly ambaye umaarufu wake ulizidi hata zaidi alipofanya hiti collabo ya Dilemma na Nelly, alikuwa amesafiri hadi Lagos, Nigeria kwa ajili kutumbuiza kwenye shoo ya This Day Festival.
Akiwa stejini mara ghafla alishindwa kumaliza shoo baada ya kuzimia na kuzirai. Alikimbizwa katika hospitali moja na kupewa huduma. Wawakilishi wake baadaye walisema kuzirai huko kulitokana na mwili wake kupungukiwa na kiwango cha maji hivyo kumnyonya nguvu hata zaidi alipokuwa akitumbuiza.
MADONNA
Februari mwaka 2015, Mwanamuziki mashuhuri wa muziki wa Pop duniani, Madonna Louise Ciccone ‘Madonna’ aliwashtua mashabiki alipodondoka katika maonyesho yake ya Tuzo la Muziki la Brit. Ingawa mwanamuziki huyo alionekana kuanguka vibaya, hakukawia kuinuka na kuendelea na maonyesho yake kana kwamba hakukuwa na jambo lolote lililofanyika.
Baada ya maonyesho hayo Malkia wa Pop alipeperusha ujumbe kupitia akaunti yake ya twitter akisema kuwa alikuwa salama na kwamba hakuna jambo linaloweza kumsimamisha. Madonna aliwashukuru mashabiki wake kwa kumtakia mema na kusema kuwa mapenzi yao yalimwinua.
BEYONCE
Aprili 2018, Mwanamuziki wa Marekani, Beyonce Knowles, alishindwa kumaliza onesho lake akiwa jukwaani baada ya kuteleza mguu wa kushoto na kuanguka pamoja na mdogo wake, Solange, katika tamasha la muziki la Coachella linalofanyika jijini Califonia, Marekani. Beyonce aliungana na Solange jukwaani kuimba wimbo wa ‘Get Me Bodied’, lakini walishindwa kumalizia baada ya kuteleza na kuanguka wakati akijaribu kumbeba