×

Kibarua cha Kocha Ndayiragije Chaota Nyasi Stars

SHIRIKISHO soka nchini, (TFF) leo Februari 11, 2021, limekubaliana kuvunja makubaliano na Kocha wa Taifa Stars, Etienne Ndayiragije.  Hii ni baada ya makubaliano ya kikao cha pamoja.

 

Katika taarifa yake, TFF imeshumkuru Ndayiragije kwa kazi yake akiifundisha Stars na kumtakia mafanikio mema aendako.

 

Aidha, TFF  imesema  itamtangaza mbadala wake baada ya mchakato wa kumpata utakapokamilika.


Leave a Comment