
ALIYEWAHI kuwa Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Bakari Mwapachu, amefariki dunia leo alfajiri Ijumaa February 12, 2021 katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili (MNH) alipokuwa akipatiwa Matibabu. Taarifa ya msiba huo imethibitishwa na Andrew Nkuzi ambaye ni msemaji wa familia ya Mwapachu.
“Balozi Bakari Mwapachu (Waziri wa zamani wa Katiba na Sheria) alizidiwa ghafla akiwa nyumbani kwake Mikocheni na alipelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu, Alfajiri leo umauti ulimfika akiwa Hospitalini hapo,” amesema Msemaji wa Familia, Bashiri Mwasora.