
ALIYEKUWA Mbunge wa Muhambwe mkoani Kigoma, Mhe. Atashasta Nditiye, amefariki dunia katika Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma leo Ijumaa, Februari 12, 2021, alikokuwa anauguzwa baada ya kupata ajali siku ya Jumatano. Kufuatia kifo hicho Bunge limeahirishwa hadi kesho saa tatu asubuhi.
Taarifa iliyotolewa na Spika wa Bunge, Job Ndugai kupitia ofisi yake imesema:
Spika wa Bunge anasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Muhambwe, Marehemu Atashasta Justus Nditiye kilichotokea leo Ijumaa tarehe 12 Feb, 2021 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa kufuatia ajali ya gari aliyoipata tarehe Februari 10, 2021 eneo la Nanene Jijini Dodoma.
Miongoni mwa nyadhifa alizowahi kushika wakati wa uhai wake ni pamoja na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.