
WAFANYABIASHARA katika Soko la Chifu Kingalu wamelalamika kwa Rais John Magufuli kuwa wanauziwa vizimba kwa bei isiyo ya manispaa na baadhi ya watu ambao wanahodhi vizimba hivyo.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Bakari Msulwa, amefuatilia na kuwabaini watumishi 16 wa manispaa hiyo waliohodhi vizimba ambao wamevirejesha baada ya kuambiwa wachague kati ya kubaki na kazi au kubaki na vizimba.
Pamoja na kurejesha vizimba hivyo, watumishi hao wamerudisha fedha walizowatoza wafanyabiashara kwa kipindi chote. Vizimba vya biashara katika Soko la Kingalu ni Tsh. 20,000 kwa mwezi ambapo watumishi hao walivihodhi na kuviuza kwa Tsh. 50,000.