
WAZIRI wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Faustine Ndungulile, Februari 24, 2021, amezindua mfumo mpya wa Simu Banking wa Benki ya CRDB katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam ambao umeboreshwa, tofauti na ule wa awali, ambapo kwa sasa unamwezesha mtumiaji wake kufungua akaunti kwa njia ya sims na kuweza kuhakikisha taarifa zake mwenyewe.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Ndungulile amesema serikali imeamua kuanzisha wizara mpya hii kutokana na ulimwengu kujikita katika teknolojia ya mtandao.

Naye Mkurungenzi Mtendaji wa CRDB Tanzania, Abdulamajid Nsekela, amesema huduma hii ya SimuBanking imefanyiwa maboresho makubwa, tofauti na awali ambapo kwa sasa inaweza kukupa fursa ya kutoa fedha kwenye ATM bila kutumia kadi.

Mbali na hivyo pia huduma hai inakuwezesha kukata bima ya gari na vitu vingine bila hata ya kuanza na zoezi la kupiga picha lakini pia haikuhitaji kwenda kwa wakala wa bima.
Huduma hii pia inakuwezesha kutoa fedha kwenye tawi lolote bila kuandika taarifa zako kwenye karatasi kwani ina njia rahisi ya kukufanya utoe kwa simu kwa namba maalum.

