×

Chama: Al Merrikh Hawatoki leo Jumamosi Sudan

KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Mzambia, Clatous Chama, amefunguka kuwa wana kila sababu ya kuhakikisha wanashinda mchezo wa leo ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kusonga mbele katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Chama ametoa kauli hiyo kuelekea katika mchezo wa tatu wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Merrikh ambao unatarajia kupigwa leo Jumamosi nchini Sudan.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Chama alisema kuwa, malengo yao ni kuona wanashinda mchezo huo ili kuweza kufuzu robo fainali kwa urahisi kutokana na ugumu wa michuano hiyo.

 

“Kitu kikubwa ambacho tunakiangalia kwenye mchezo wa kesho (leo) ni kuweza kupata matokeo, tunajua mechi itakuwa ngumu kwa kuwa tunacheza ugenini lakini uzoefu wetu utakuwa chachu kubwa ya kuweza kupata kile ambacho tumekifuata huku.

 

“Wapinzani wetu kwanza hawana timu dhaifu kama inavyochukuliwa na wengi kwa kuwa wamepoteza mechi mbili zilizopita lakini bado tuhawaheshimu kwa kuwa tunacheza nao michuano hii pamoja, naamini hawataweza kutoka kwa kuwa tumejipanga kupata matokeo hapa,” alisema Chama.

STORI: IBRAHIM MUSSA, Dar es Salaam

Leave a Comment