
RAIS wa klabu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Patrice Motsepe, anatajwa kuwa Rais Mpya wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) baada ya Ahmad Ahmad, katika kuelekea uchaguzi mkuu wa CAF March 12 2021 nchini Morocco.
Inaripotiwa na waandishi mbalimbali wa Afrika kuwa Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) Gianni Infantino, amewashauri Jacques Anouma, Augustin Senghor na Ahmed Yahya kujitoa na kumuunga mkono Motsepe ili amshinde Ahmad.
Taarifa zilizopo zinasema Infantino na Ahmad ‘haziivi’ tena na sasa na Infantino anatumia nguvu nyingi kuhakikisha Ahmad harudi tena madarakani baada ya jaribio la kumfungia kugonga mwamba kwa Mahakama ya Kimichezo Duniani (CAS) kutengua uamuzi wa FIFA.