×

Global Habari Machi 07 – Mama Samia Suluhu Atoa Wito Siku Ya Wanawake

Katika kuelekea siku ya wanawake Duniani Machi 8 mwaka huu, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan Ametoa wito kwa wadau kutoa elimu katika maeneo mbalimbali ili kupinga mila potofu za ukandamizaji wa mtoto wa kike kwa maslahi ya Taifa zima kwa ujuma Makamu wa Rais ameyasema hayo katika hafla ya harambee ya kuchangia mtoto wa kike kielimu kwa lengo la kumuhamasisha kujiunga na kusoma kwa bidii masomo ya sayansi, hafla iliyofanyika Visiwani Zanzibar.

Leave a Comment