×

Denmark Yasitisha Chanjo ya Covid 19

NCHI ya Denmark,  imesitisha utoaji wa chanjo ya Oxford-AstraZeneca kwa muda wa wiki mbili ili kuchunguza ripoti za baadhi ya wagonjwa kupata tatizo la damu kuganda siku chache baada ya kupatiwa chanjo hiyo.

 

Waziri wa Afya amesema wamechukua hatua hiyo jana Machi 11, ikiwa sehemu ya tahadhari ili kuchunguza endapo kuna madhara zaidi yaliyojitokeza tofauti na la damu kuganda.

 

Mamlaka ya Afya ya Denmark imesema uamuzi wa kusimamisha chanjo ya AstraZeneca umekuja baada ya mwanamke wa miaka 60 nchini humo kupewa dozi ya na kupoteza maisha.

 

Mpaka sasa  nchi sita duniani zimesitisha matumizi ya chanjo ya AstraZeneca kutokana na madhara mbalimbali, nchi hizo ni Austria, Estonia, Lithuania, Luxembourg, Latvia na Denmark.

 

Zuio hilo limekuja wakati ambao nchi ya Austria imezuia chanjo hiyo ili kupisha uchunguzi baada ya mtu mmoja aliyetumia chanjo hiyo kufariki dunia.

Leave a Comment