×

Baada ya Shinikizo la Umoja wa Ulaya, Serbia Yagoma Kuiwekea Vikwazo Urusi

Rais wa Serbia Aleksandar Vuvic akiwa na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz

RAIS wa Serbia Aleksandar Vuvic amegoma wito kutoka kwa Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz kuhusu kuiwekea vikwazo Urusi kutokana na kitendo chake cha kuivamia Ukraine.

 

Mapema Scholz alisema Serbia ambayo ipo katika harakati za kujiunga na Umoja wa Ulaya inatakiwa ioneshe mfano kwa kuiwekea vikwazo Urusi kutokana na kuivamia Ukraine.

Kansela Scholz alitembelea nchi ya Serbia hivi karibuni

“Kuhusiana na suala la vikwazo hapa kila mtu ana mtazamo wake, tunakumbuka vikwazo kwa upande wa Serbia lakini tunasahau kuwa vikwazo pekee havitoshi.” Alisema Vuvic.

 

Serbia ipo katika wkati mgumu kutokana na uhusiano wake wa muda mrefu na Urusi kiasi kwamba inawia vigumu kwa Taifa hilo kubadili uamzui na kuiwekea vikwazo Urusi.

 

Kwa upande mwingine Mke wa Rais wa Ukraine Volodymir Zelensky anayefahamika kwa jina la Olena Zelenska amesema jumla ya wanawake 3,700 wa Ukraine wameshajiunga na jeshi la nchi hiyo.

Olena Zelenska Mke wa Rais wa Ukraine Volodymir Zelensky

Olena amesema kati yao wanawake 1000 tayari wameshakuwa makamanda, amenukuliwa akisema:

“Madaktari wetu wengi ni wanawake, kama ilivyo zaidi ya asilimia 50 ya wajasiriamali wanaofanya kazi kusaidia jeshi letu kiuchumi.”alisema Zelenska.

 

 

 

 

 

Leave a Comment