
Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa, leo Ijumaa, Machi 12, 2021, amewataka Watanzania wote wawapuuze wapotoshaji wa mitandaoni wanaotaka kuleta taharuki juu ya Afya ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.
Akizungumza baada ya Swala ya Ijumaa katika Msikiti Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Waziri Mkuu Majaliwa amesisitiza kuwa tabia ya Watanzania wenzetu wanaoishi nje ya nchi ya kupotosha makusudi mambo mbalimbali yanayohusu maendeleo ya nchi pamoja na Kuzusha Uongo.
“Kuna wenzetu hawaishi hapa nchini, wao kazi yao ni kutuombea mabaya tu, kupandikiza chuki tu. Sasa unamuombea mwenzako kufa hiyo ni akili kweli? Nawatoa hofu Watanzania wote, Rais wenu yuko imara anafanya kazi zake kama kawaida za ofisini.
“Rais ana shughuli nyingi, Wanataka atoke aende wapi, Kariakoo au Magomeni tangu lini? Leo Asubuhi wakati nakuja huku nimeongea nae kwa simu na ameniagiza niwaambie wana njombe kuwa anawapenda sana na anawashukuru sana kwa kura nyingi mlizompigia,” mesema Majaliwa.
Aidha, Waziri Mkuu Majaliwa amewataka watanzania Kuwaombea Viongozi wakuu wa nchi kwani wana Dhamana kubwa ambayo wamepewa na Watanzania ya kuwatumikia.