×

RC Chalamila: Rais Magufuli Haumwi, Nimeongea Naye – Video

MKUU wa mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila, amesema amempigia simu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, na kumshukuru kwa ajili ya miradi kadhaa aliyoipokea mkoani kwake na kumweleza kuwa haumwi ni mzima wa afya na anaendelea na majukumu yake Ikulu.

 

 

RC Chalamila amesema hayo leo Ijumaa, Machi 12, 2021 na kuwataka watu wenye nia ovu kuacha kumzushia Mhe. Rais kuwa anaumwa kwani Rais ni mzima na anaendelea na majukumu yake ya kuijenga Tanzania.

 

“Imetrend kwamba Rais yupo kwenye matibabu mahali fulani, niwaambie Rais yupo imara na anaendelea na kazi. Leo asubuhi nimempigia simu Rais (John Magufuli), kumshukuru kwa fedha alizotupa za kutekeleza miradi ya maendeleo na amenijibu kwa furaha na faraja. Wanaozungumza Rais yuko kwenye matibabu labda wao wako kwenye matibabu,” amesema Chalamila.

 

Kwa upande mwingine, Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa amewataka Watanzania wawapuuze Wapotoshaji wa mitandaoni wanaotaka kuleta taharuki juu ya Afya ya Rais. “Rais ana shughuli nyingi, wanataka atoke aende wapi, Kariakoo au Magomeni tangu lini?”

 

Leave a Comment