×

Sheria za TZ Zaanza kutafsiriwa kwa Kiswahili

Wataalamu wa #Sheria kutoka Taasisi mbalimbali wakiongozwa na Wanasheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria wameanza kazi ya kutafsiri Sheria zote Nchini.

 

Kutokana na Sheria kuwa Sekta inayomsaidia Mtu kupata haki, Serikali iliagiza Lugha ya Kiswahili itumike katika masuala mbalimbali ya kisheria kisha lugha nyingine ziwe ni za nyongeza, ili kuwezesha Wananchi kuelewa kwa urahisi kuhusu kesi zao.

 

Zoezi hili la kutafsiri Sheria litafanyika kwa Awamu Tatu kabla ya kuhakikiwa kwa tafsiri hizo kama kilichotafsiriwa ni sahihi na hakijapoteza maana ambapo zoezi hili linatarajiwa kukamilika mwezi Desemba 2021.

 

 

Leave a Comment