×

Tulia Mgeni Rasmi Pambano la Queen of The Ring

NAIBU Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Akson anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika pambano la kumsaka malkia wa ulingo (Queen of the Ring) Machi 27 2021 Ubungo Plaza Dar es salaam.

 

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mratibu wa matukio Mwantum Mgonja alisema wameshamtumia barua kinachosubiriwa ni majibu.

 

“tunasubiria majibu ila tunaimani atakubali na kuwa mgeni rasmi katika pambano la ngumi za kulipwa kwa wanawake” alisema Mwantum.

 

Aliongeza kuwa pambano hilo ni la kihistoria litawakutanisha  wanawake maarufu wa ngumi lakini pia wanawake kucheza mkanda mkubwa kwa raundi kumi.

 

“wanawake tunaweza sasa kudhihirisha hilo pambano la kihistoria la masumbwi linakuja na litakuwa la mfano na tunatumaini mgeni rasmi atatukubalia ombi letu” alisema Mwantum.

 

Leave a Comment