
TAARIFA: Marais zaidi ya 10 kumuaga Dkt. John Pombe Magufuli Uwanja wa Jamhuri kesho Machi 22, 2021 Dodoma. Orodha na taarifa kamili itatolewa leo saa nane kamili mchana katika mkutano wa Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt Hassan Abbas na waandishi wa habari. Tuendelee kumuombea kiongozi wetu na kuliombea Taifa letu.