×

Askofu Bendera Asimulia Ndoto Aliyoota Kabla ya Kifo cha Magufuli – Video

ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Ufunuo, Mchungaji Paul Bendera alipata ndoto ya kiroho kabla ya Rais wa sasa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan kutangaza kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.

 

Askofu Bendera amesema hayo juzi Jumapili kwenye ibada ya misa wakati akiwahubiria waumini wake na kuongeza kuwa baada kujiwa na ndoto hiyo, Jumapili yake aliamua kusimamisha waamini wake kanisani hapo kufanya maombi maalum kwa taifa.

 

Aidha, Bendera amesema kuwa roho ikifika mwisho hubadilika na kuanza kutoa maneno ya wosia hivyo amewataka waumini wake na Watanzania kumshukuru Mungu kwa zawadi ya Rais Magufuli huku akiwataka pia kuishi kwa kutenda matendo mema yampendezaye Mungu ili siku ya mwisho awapokee katika ufalme wake.

 

Leave a Comment