×

Slaa: Kipaumbele cha JPM Kilikuwa Kuwainua Watanzania

BALOZI wa Tanzania nchini Sweden, Dkt. Wilbroad Slaa leo Machi 24, amesema kipaumbele cha Hayati Rais John Magufuli kilikuwa kuwainua Watanzania, na njia alizoweka hadharani kutimiza hilo ni kuwekeza kwenye Viwanda pamoja na Uwekezaji.

Ameeleza, “Wakati naapishwa kauli yake ilikuwa nendeni mkafanye Diplomasia ya Uchumi, maana yake ni kutafuta wawekezaji, watu wenye viwanda vikubwa na watakaoingia kwenye ushirikiano na Watanzania katika kuuziana bidhaa mbalimbali”.

Aidha, Dkt. Slaa amesema kuleta Wawekezaji pekee haitoshi kama hakuna watu wa upande wa Tanzania kushirikiana akiongeza Biashara lazima iwe pande mbili.

 

Dkt. Slaa ameshiriki kutoa heshima za mwisho kwa Hayati Dkt. John Magufuli kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.

 

Leave a Comment