×

Ufugaji Sungura Fedha Njenje

NI jasiri pekee ndiye anayeweza kushinda changamoto za maisha magumu.Kadiri siku zinavyokwenda baadhi ya watu wameanza kupoteza ujasiri na kuanza kulialia kwamba maisha yamekuwa magumu.

 

Baadhi ya watu hao wamekuwa wanajiuliza wafanye nini ili waweze kupiga fedha nyakati hizi.Pengine nikukumbushe msomaji wangu kuwa ujasiri ni mali chukua hatua za kukabiliana na maisha magumu bila kukata tamaa.

 

Leo katika safu hii nakuletea fursa ya ufugaji wa sungura ambayo inaweza kukukomboa kimaisha haraka.Uzalishaji na ufugaji wa sungura ni shughuli ya kiuchumi inayokua kwa kasi kubwa.

Sungura huzaliana ndani ya kipindi cha miezi miwili tu.Sungura huzaa watoto sita hadi 10 kwa mkupuo wa kwanza. Huzaa pia watoto 10 hadi 15 kwa mkupuo wa pili.Jiulize ukiwa na majike watatu ndani ya muda huo unaweza kuwa umepata sungura wangapi?

 

Utafiti uliowahi kufanywa na taasisi moja ya Marekani, unaonesha ili kupata nyama kilo 150 ya ng’ombe unahitaji ekari mbili za malisho lakini ili kupata kilo hizo za sungura unahitaji hatua tano kwa tano. Umeona jinsi ilivyo rahisi kufuga sungura?

 

Kingine ni kwamba nyama ya sungura ipo katika kundi la nyama nyeupe ambayo watu wengi wanashauriwa kula kwa afya. Haina lehemu kama ilivyo kwa ng’ombe na mbuzi.

 

Pia haina kemikali hatarishi.Kadiri siku zinavyokwenda nyama ya sungura imeanza kuwa na soko la kutosha tofauti na zamani.Ufugaji wa sungura umepanda chati siyo tu kwa ajili ya nyama, bali pia, mkojo wake ni dili, kwani hutumika kama viuatilifu.

 

Sungura jike akilishwa vizuri, anaweza kuzaa mara sita ambapo kila uzao anaweza kuzaa watoto sita hadi 10 na mara sita ni sawa na kuzaa sungura 36 hadi 60.Hivyo kwa jozi moja ya sungura dume mmoja na majike sita, tegemea kupata sungura 216 hadi 360 kwa mwaka, pasipo kuongeza jozi nyingine ya wazazi.

 

Sungura hubeba mimba kwa siku kati ya 26 hadi 31, na anatumia saa nne hadi sita kuzaa watoto alionao tumboni kama ni 10 hadi 15, ambao huzaa mmoja baada ya mwingine.Kama wanyama wengine, baada ya kuzaa huwalamba na watoto huanza maisha wakitafuta matiti ya mama wanyonye.

 

Jambo jema katika ufugaji wa sungura ni kwamba wanyama hawa hawahitaji eneo kubwa la kufugia na hula vyakula mbalimbali vinavyoliwa na binadamu yakiwemo majani mbogamboga ambayo ni rahisi kuyapata.Kwa mujibu wa uchunguzi wa soko ni kwamba sungura mmoja huuzwa kati ya shilingi 15,000 hadi 20,000.

 

Hebu chukua hatua ya kuchangamkia furasa hii ambayo inaweza kukupa mkwanja chapuchap. Kumbuka sungura unaweza kufuga kwa kujenga ban

Leave a Comment