×

Teni The Entertainer Aachia Dude ‘Wondaland’

MWANAMUZIKI staa nchini Nigeria, Teni The Entertainer ameachia albamu yake mpya ya muziki inayokwenda kwa jina la “Wondaland”, ambayo kwa mara ya kwanza imeachiwa sokoni Machi 19, mwaka huu.

 

 

Albamu hiyo mpya imefungua mafanikio mapya kwa staa huyo ulimwenguni, ambapo miongoni mwa singo zinazofanya vizuri zaidi kwa sasa ni pamoja na “For You” aliopiga kolabo na msanii hot cake nchini Nigeria, Davido.

 

 

“For You” umetazamwa na zaidi ya watu 14 milioni na kwa sasa ndiyo wimbo unaoshikilia nambari moja kwenye chati ya muziki za Apple Music Nigeria, lakini ukiendelea kufanya vizuri hata nje ya Nigeria.

 

 

Aidha, wimbo huo upo kwenye 10 Bora za nyimbo bora za Afrobeats zinazochezwa nchini Uingereza, huku ikiwa kwenye 20 Bora kwenye nyimbo zinazosikilizwa ulimwenguni kote.

Kutazama Teni WONDALAND:

Kuzatama Teni & Davido – For You:

Baada ya Teni kufanya kazi kwa miaka miwili katika miji saba kote ulimwenguni ikiwemo, London (Uingereza), New York (Marekani), Dubai (Falme za Kiarabu), Orlando (Marekani), Ondo (Nigeria), Lagos na Abuja (Nigeria).

 

 

Teni aliona albamu hiyo kama kazi ya upendo na kitu ambacho kitampa msikilizaji burudani ya aina yake kuanzia wimbo wa kwanza hadi wa mwisho katika albamu hiyo.

 

 

Teni anasema: “Nilitaka kutoa albamu ambayo kila mmoja kutoka katika mji wa ardhi ya mama yangu, Ondo au mji wa baba yangu – Ekiti mpaka Osaka, Japan wanapata burudani ya aina yake, lakini pia elimu kupitia albamu hiyo.

 

 

“Nina imani albamu hii inaweza kuishi na kusikilizwa hata kwa miaka zaidi ya 20 ijayo, kutokana na ujazo na ubora uliomo ndani yake.”

 

Staa huyo anamiliki tuzo kadhaa za muziki zikiwemo za Mwimbaji Bora, Mwandishi Mashairi Bora, Mtumbuizaji Bora na nyingine nyingi nchini humo.

 

 

Anamalizia kwa kusema: “Ni albamu ambayo haichoshi kuisikiliza. Siyo kwamba ni nzuri kwa sababu inatoka kwa msanii wa Kiafrika, bali kwa sababu ni muziki safi na zawadi ya pekee kutoka ndani kabisa ya moyo wangu.

“Nimekuwa nikiifanyia kazi hii albamu kwa miaka miwili katika miji saba ulimwenguni – London, New York, Orlando, Dubai, Ondo, Lagos na Abuja. Lengo ni kupata mchanyato mzuri ambao utakonga nyoyo za wasikilizaji wangu – na ndicho nilichokifanya.”

 

Na Mwandishi Wetu

Leave a Comment