×

Balozi Katanga: Nilipata Taarifa za Uteuzi Nikiwa Airport

KATIBU Mkuu Kiongozi, Balozi Hussein Katanga leo Alhamisi Aprili Mosi, 2021 amesema alipokea taarifa kuwa ameteuliwa kushika wadhifa huo akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) akisubiri ndege kwenda jijini Dodoma.

Balozi Katanga ameyasema hayo  mara baada ya kula kiapo Ikulu ya Chamwino, Dodoma.

Amesema kwa imani kubwa ambayo Rais Samia ameionyesha kwake kwa kumteua, atafanya kazi kwa maelekeo yake na kwa mujibu wa kiapo.

 

“Leo nilikuwa nirudi Japan kwa maelekezo ya katibu mkuu wizara ya nchi za nje na tiketi ile ya Japan ikabidi niahirishe kwa sababu jana majira ya saa 6 nikachukuliwa natakiwa kufuata maelekezo nenda huku, ongoza huku nikafika uwanja wa ndege paki gari pale, mambo mengine utayakuta hukohuko Dodoma.”

 

“Nilikuwa naangalia televisheni nikayajua kabla sijafika Dodoma nashukuru na walioniongoza nikawahi kufika katika shughuli hii, kazi ya katibu mkuu kiongozi ni kuunganisha ili Serikali ifanye kazi na hizi wizara na taasisi zake zimewekwa ili kuleta ufanisi na utaaluma,” amesema.

 

Balozi Katanga amesema Serikali inayotaka kufika dira ya 2025 inatakiwa ifanye kazi pamoja, na kwamba ushirikiano ni jambo muhimu na wizara zinategemeana, “lazima kuhakikisha tunalifanyia kazi.”

Leave a Comment