
Wabunge wateule watatu walioteuliwa jana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia ambao ni Dkt. Bashiru Ally, Balozi Liberata Mulamula na Mbarouk Nassor Mbarouk, leo Aprili 1, 2021 wameapa kuwa wabunge wa Bunge la Tanzania.
“Niwapongeze sana waheshimiwa mawaziri na manaibu wote kwa kubaki kwenye baraza na huo ndo uzuri wa mama, amekuwa ‘considerate,’ wangekuwa wengine upewe panga hilo majeruhi wangekuwa kibao.

“Yapo mambo mengi yakufanya kila mmoja kwenye wizara yake na mengi sana mtayapata kama ushauri kutoka kwa wabunge cha msingi nyinyi ni wabunge kama sisi, hapa bungeni ndio nyumbani huko mmeenda kama matembezi.

“Suala la kukosekana kwa dawa sio la jana au juzi, ni la siku nyingi kila tukikaa msd hivi, kwanini wizara ya fedha msichukue hilo deni la msd ili fedha zinazopelekwa msd zitoe dawa, na nyinyi mtajuana na msd kwa aina yenu” amesema Job Ndugai, Spika wa Bunge.
Aidha Spika wa Ndugai ameahirisha Bunge hadi siku ya Jumanne Aprili 6 saa 3:00 asubuhi.