Dkt. Mpango Awafariji Watoto, Wazee, Wenye Mahitaji Maalum
Global Publishers April 5, 2021 0 Comments
SHARE THIS:
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango amelishukuru Shirika la Teresia wa Mtoto Yesu lenye Makao Makuu yake Nchini india kwa kazi nzuri wanayoifanya kuisaidia Tanzania katika kazi ya kuwatunza Watoto Yatima, Wazee pamoja na Watu wenye Mahitaji maalum.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akizungumza jambo na Paroko wa Parokia ya MT. Theresia wa Watoto wa Yesu Kanisa Katoliki Jimbo Kuu Nzinje Dodoma Padri Binoy Thomas, baada ya kumalizika Ibada ya Misa Takatifu ya Jumatatu ya Pasaka leo April 05, 2021.
Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Mpango ameyasema hayo leo April 05,2021 katika Kituo cha Kuwatunza Watoto Yatima, Wazee pamoja na Watu wenye Mahitaji Maalum cha Huruma Missionary Sisters of charity kiliopo Hombolo jijini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akifurahia jambo na Mtoto Gilbert Mezi ( 11) anaelelewa na kutunzwa katika Kituo cha Huruma Missionary Sisters of Charity Hombolo Dodoma wakati Makamu wa Rais alipofika katika Kituo hicho leo April 5, 2021 kwa ajili ya kuwafariji pamoja na kuwapa Chakula, Vinywaji na Fedha Taslim kwa ajili ya Sikuu ya Pasaka.
Aidha Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango amesema atawahimiza Wizaya ya Afya na Maendeleo ya Jamii kitengo cha Ustawi wa Jamii wafike katika Kituo hicho waweze kufanya kazi ya kutoa huduma Zaidi.
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Jenisia Mpango, akifurahia jambo na Mtoto Gilbert Mezi ( 11) anaelelewa na kutunzwa katika Kituo cha Huruma Missionary Sisters of Charity Hombolo Dodoma wakati alipofika katika Kituo hicho leo April 5,2021 kwa ajili ya kuwafariji Watoto, Wazee na Watu wenye Mahitaji Maalum wanaotunzwa katika Kitu hicho ikiwa ni maadhimisho ya Jumaatatu ya Pasaka.
Kituo hicho kinachotunza Watoto Yatima, Wazee, pamoja na Watu wenye Mahitaji Maalum kina Jumla ya Watu 90 wenye Uhitaji wa aina mbalimbali.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango na Mkewe Mama Jenisia Mpango wakiwaangalia Watoto wanaolelewa na kutunzwa katika Kituo cha Huruma Missionary Sisters of Charity Hombolo Dodoma wakati walipotembelea katika Kituo hicho leo April 5, 2021 kwa ajili ya kuwafariji pamoja na kuwapa Chakula, Vinywaji na Fedha Taslim kwa ajili ya Sikuu ya Pasaka. kushoto ni Paroko wa Parokia ya MT. Theresia wa Watoto wa Yesu Kanisa Katoliki Jimbo Kuu Nzinje Dodoma Padri Binoy Thomas.
Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango amefika katika kituo hicho kwa ajili ya kuwafariji pamoja na kutoa vifaa mbalimbali ikiwemo Chakula, Sabuni, Vinywaji na fedha Taslim Shilingi Milioni Tano, kwa ajili ya Sikukuu ya Pasaka, ambapo pia amewasilisha salam za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuwatakia Watanzania wote heri ya Sikukuu ya Pasaka na kuendelea kufanya kazi ili kuweza kuijenga Nchi yetu ya Tanzania.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akifurahia jambo na Mtoto Ali Mwaka (1) anaelelewa na kutunzwa katika Kituo cha Huruma Missionary Sisters of Charity Hombolo Dodoma wakati Makamu wa Rais alipofika katika Kituo hicho leo April 5, 2021 kwa ajili ya kuwafariji pamoja na kuwapa Chakula, Vinywaji na Fedha Taslim kwa ajili ya Sikuu ya Pasaka.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akikabidhi Vifaa mbalimbali ikiwemo Chakula na Vinywaji, Fedha Jumla ya Shilingi Milioni Tano kwa Sister. M. Prodencia M. C wa Parokia ya MT. Theresia wa Watoto wa Yesu Kanisa Katoliki Jimbo Kuu Nzinje Dodoma, kwa ajili ya Sikukuu ya Pasaka kwa Watoto Yatima, Wazee na Watu wenye Mahitaji Maalum wanaotunzwa katika Kituo cha Huruma Missionary Sisters of Charity Hombolo Dodoma leo April 5, 2021.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango na Mkewe Mama Jenisia Mpango wakiwa katika Picha ya Pamoja na Watoto, Wazee pamoja na Watu wenye Mahitaji Maalum, wakati walipowatembelea katika Kituo chao cha Huruma Missionary Sisters of Charity Hombolo Dodoma leo April 5, 2021 kwa ajili ya kuwafariji pamoja na kuwapa Chakula, Vinywaji na Fedha Taslim kwa ajili ya Sikuu ya Pasaka.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango na Mkewe Mama Jenisia Mpango, Paroko wa Parokia ya MT. Theresia wa Watoto wa Yesu Kanisa Katoliki Jimbo Kuu Nzinje Dodoma Padri Binoy Thomas na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda, wakiwa katika Picha ya pamoja baada ya kumalizika Ibada ya Misa Takatifu ya Jumatatu ya Pasaka leo April 05, 2021. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)