×

Rais Samia Kuunda Tume ya Covid-19 – Video

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu amesema anatarajia kuunda kamati ya wataalamu ambayo itamshauri kuhusu hatua sahihi za kuchukua kuhusu ugonjwa wa #COVID19.

 

 

Samia amesema hayo leo Jumanne, Aprili 6, 2021, wakati akihutubia taifa mara baada ya kuwaapisha Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Wakurugenzi na Wakuu wa Idara aliowateua juzi na kusema kuwa Tanzania haiwezi kujitenga kama kisiwa, na kwamba lazima ijulikane wazi kama inakubaliana na hatua za dunia au inazikataa.

 

 

“Nakusudia kuunda Kamati ya wataalamu kuliangalia suala la Covid-19, waliangalie kwa upana wake, kuhusu tiba zetu, Tanzania sio kisiwa, lakini pia hatuwezi kukubali kila tutakacholetewa bila ya kufanya utafiti wa ndani.

 

 

“Kamati ya Wataalamu wakae waliangalie kwa upana wake kitaalamu kisha watushauri Serikali, halifai kulinyamazia aidha, ili tujue tunalikataa au kulikubali kwa Tafiti za kitaalamu, watupe upeo wa tatizo hili lilivyo na hayo yanayopendekezwa na ulimwengu.

 

 

“Hatuwezi kujitenga kama Kisiwa na hatuwezi kupokea kila tunacholetewa, Rais Kikwete alituambia akili za kuambiwa changanya na zako, tuwe na msimamo unaoeleweka, sio tunasoma tu mambo ya Covid-19 Ulimwenguni, Tanzania deshi deshi haieleweki,” amesema Samia.

🔴#LIVE​​: RAIS SAMIA AWASHA MOTO, AWAAMBIA VIONGOZI – “NIKIKUTANA NA BANGO MOJA, DED, DC MNAONDOKA”

Leave a Comment