
JAMAA anaitwa Rico “Orc” Ledesma (41) jamaa wa nchini Brazil ambaye alibadili moja kwa moja mwili wake kuwa kama dubwana au shetani ameanza kupata ofa za kuigiza filamu za kutisha Hollywood nchini Marekani.

Rico alianza kuubadili kwa tattoo mwili wake miaka 7 iliyopita, aliupasua ulimi wake, kuchorwa tattoo machoni, kukatwa sehemu ya masikio yake, kutobolewa pua na kupandikizwa pembe mbili mdomoni.
Pembe hizo pekee zilimgharimu £400 zaidi ya million 1 ya Kibongo ingawa kwa jumla gharama za kujibadili Ni kubwa lakini alisaidiwa na mpenzi wake kwa jina la Krishna (25) ambaye ni mtaalamu wa kutoboa miili.

Yeye na Krishna walikutana mitandaoni na kupendana Kisha kuzaa mtoto wa kike na Sasa wanatarajia kupata mtoto wa pili.

Amesema kujibadili mwili wake moja kwa moja kuonekana Kama dubwana flani ilikuwa moja ya malengo yake kimaisha na sasa yameanza kuzaa matunda kwa kuanza kupata attention toka kwa watengenezaji filamu za kutisha Hollywood.