
Kocha wa Mabingwa wa Kihistoria Ligi Kuu soka Tanzania Bara, Juma Mwambusi ameahidi ushindi kwenye mchezo wao wa hapo kesho dhidi ya vijana wa Kinondoni timu ya KMC FC.
”Kila mechi tunayocheza itakuwa fainali, maanadalizi tuliyofanya kesho yatakuwa kioo kuonyesha tumejiandaa vipi kwa mapumziko baada ya kuondokewa na Mhe. marehemu Rais John Pombe Magufuli kwakweli ilitugusa kama wanamichezo na Watanzania kwa ujumla.” – Kocha wa Yanga Juma Mwambusi.
”Pamoja na maombolezo tulikuwa tukijiandaa kuhakikisha baada ya maandalizi hayo tuwape kile Yanga, wananchi wanachokitaraji. Kwa hiyo tunasema kesho tupo tayari kwa mapambano.”
Yanga inatarajia kushuka uwanja wa Mkapa majira ya saa 1:00 usiku kuwakabili KMC FC huku wakiwa ndiyo vinara wa Ligi Kuu na lengo lao kubwa mwaka huu ni kuubeba Ubingwa huo wa VPL.