×

India Yarekodi Visa Zaidi 200,000 Katika Saa 24

INDIA imeingia kwenye rekodi baada ya kurekodi visa zaidi ya  200,000 vya ugonjwa wa Covid 19, ndani ya masaa 24, idadi kubwa zaidi kuwahi kutokea tangu ugonjwa huo kuingia nchini humo.

 

Taifa hilo linakabiliwa na wimbi jipya la maambukizi ambalo kitovu chake ni Maharashtra, eneo lilipo Jiji la Mumbai, zaidi ya robo ya maambukizi ya India yametokea eneo hilo.

 

Tayari watu 173 123 wamepoteza maisha kutokana na Covid 19 huku Hospitali nyingi zenye wagonjwa wa Virusi vya Corona zikiripoti uhaba wa vitanda na Oxygen

Taifa hilo ambalo lina idadi kubwa ya watu  duniani, kwa ujumla kuna visa mil. 14 ugonjwa huo.

 

Visa nchini humo vilianza kupungua mwishoni mwa mwaka 2020,  lakini idadi ilianza kuongezeka tena katikati ya mwezi Februari mwaka huu.

 

Kampeni ya utoaji chanjo ilianza Januari na kwa mujibu wa Wizara ya Afya, zaidi ya dozi Milioni 111 za Chanjo zimetolewa.

 

Leave a Comment