×

Visima Hivi Kupunguza Shida ya Maji Buchosa

KAZI ya uchimbaji wa visima inaendelea katika Vijiji vya Jimbo la Buchosa ili kutimiza ahadi ya Mbunge wa Jimbo hilo, Mhe. Eric Shigongo aliyoitoa kwa wananchi wakati wa kampeni zake mwaka jana.

Visima hivyo vinachimbwa katika maeneo mbalimbali ya vijiji vya Jimbo la Buchosa ambapo jana zoezi hilo limeendelea katika Kijiji cha Bupandwa ambapo kinachimbwa kisima kirefu chenye kina zaidi ya mita 100.

Hii itasaidia kupata maji ya uhakika ambayo yatahudumia wakazi wa Bupandwa na vitongoji vyake na kupunguza adha ya wananchi wa Kijiji hicho kufuata maji umbali mrefu.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Eric Shigongo (@ericshigongo)

Leave a Comment