×

Ajali ya Treni Yaua Watu 11

Watu 11 wamefariki dunia na wengine 98 wamejeruhiwa katika ajali ya treni iliyotokea karibu na mji mkuu wa Misri, Cairo.
 
Mamlaka ya Reli nchini Misri imesema kuwa, treni hiyo iliyokuwa na mabehewa manne ilikuwa ikisafiri kutoka Cairo kuelekea jimbo la Mansoura na ndipo ilipoacha njia na kuanguka.

 

Dereva wa treni hiyo pamoja na wasaidizi wake wanane wamekamatwa kwa uchunguzi, kwa mujibu wa gazeti la Al-Shorouk, Misri imekuwa ikishuhudia ajali za mara kwa mara za treni.

 

Mapema wiki iliyopita, watu 15 walijeruhiwa baada ya treni nyengine kuacha njia katika jimbo la kaskazini la Minya al-Qamh, 26 Machi, treni mbili za abiria ziligongana kusini mwa nchi hiyo na kuuwa watu 19.

 

Mwezi Februari 2019, ajali ya treni ilisababisha vifo vya watu 31.

 

Leave a Comment