
Rais Samia Suluhu Hassan, amekutana na kufanya mazungumzo na mkurugenzi mkazi wa Benki ya Dunia, Mara Warwick.
Katika mazungumzo hayo, Rais Samia ameishukuru Benki ya Dunia kwa kuendelea kuwa mshirika mzuri wa maendeleo ya Tanzania na amemhakikishia kuwa serikali itaendelea kukuza uchumi na kuinua ustawi wa wananchi wa Tanzania.

Rais Samia, ameiomba Benki ya Dunia kuendelea kushirikiana na Tanzania katika kujenga uchumi utakayoyagusa makundi yote ya jamii hususan kuwafikia watu maskini, kuboresha huduma za kijamii, kuwawezesha wanawake kiuchumi na kujenga mifumo ya kidijitali itakayorahisisha utendaji kazi ikiwemo ukusanyaji wa mapato.

