×

Senzo Naye Aibuka, Amfungukia Kocha

MSHAURI wa masuala ya mabadiliko ndani ya Klabu ya Yanga, Senzo Masingiza amesema kuwa wanaimani na kocha mpya Nasreddine Nabi kuwa ataipatia mafanikio timu hiyo kulingana na uwezo wake mkubwa na uzoefu alionao.

 

Nabi, raia wa Tunisia alitua nchini wiki hii Jumanne na kusaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu wa kukinoa kikosi cha Yanga.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Senzo alisema kulingana na uwezo mkubwa na uzoefu alionao kocha mpya wa timu hiyo Nasreddine Nabi, wanaimani atawasaidia katika kuipa mafanikio timu hiyo ambayo wanayatafuta kwa muda mrefu.

“Huyu ni kocha mzuri sana, kafundisha Congo, Sudan na timu nyingine pia ana makombe mengi ndani ya timu nyingi ambazo amezifundisha, hivyo tunaamini uzoefu mzuri alionao utatusaidia sana.

 

“Kwa klabu kama Yanga tumefurahi kumpata kocha kama huyu, kama ambavyo mmeona tulikuwa na presha ya makocha waliopita kulingana uhitaji wa timu, tunatarajia kupata kilicho bora kutoka kwa kocha huyu mpya,” alisema Senzo.

Marco Mzumbe, Dar es Salaam

Leave a Comment